Sarufi Ya Kiswahili Pdf

Sarufi Maumbo Ya Kiswahili

Mofimu katika sarufi ni jina la sehemu ndogo kabisa yenye kuwakilisha maana. Mifumo ya elimu rasmi. Mofimu ni kipashio kidogo kuliko vyote katika lugha chenye maana. Sarufi Zalishi - ebookdig.biz is. Nadharia Ya Sarufi Geuza Maumbo Zalishi PDF Autumn Leaves. Fonolojia Ya Nomino-mkopo Za Kikamba Kutoka Kiswahili.

Misingi ya Sarufi ya Kiswahili by • ISBN: 403 • SKU: 009 Misingi ya sarufi ya lugha yoyote ile huwa katika Mofolojia (muundo wa maneno), Fonetiki (sauti), Sintaksia (muundo wa sentensi), Semantiki (maana) na Isimu (dhana ya lugha) yake. Kitabu hiki kimeishughulikia misingi hii katika muktadha wa Kiswahili.

Kwa mara ya kwanza vipengele vyote husika vimeelezwa na kuchambuliwa kwa Kiswahili. Matokeo ni johari ambayo itawafaa wanafunzi wa Shule za Upili, Vyuo vya Walimu na Vyuo Vikuu. Vilevile, wapenzi wa lugha watanufaika kutokana na maelezo mwafaka ya muundo na ufanyikazi wa Kiswahili.

Sarufi ya Kiswahili na sintaksia ni kozi inayochambua sarufi ya Kiswahili kwa kuzingatia nadharia za sintaksia kama zilivyoasisiwa na wanazuoni wa isimu. Sintaksia ni tawi la isimu linalohusu namna maneno yanavyounda virai na sentensi za Kiswahili. Sintaksia inahusu tungo za lugha ambazo zaweza kuwa ni maneno, virai, vishazi na sentensi. Japokuwa neno ni kipashio cha maumbo, linasadifu kuingia katika sintaksia ya lugha kwani lenyewe lina muundo wake unaotokana na viambajengo vinavyoliunda ambavyo ni mzizi na viambishi. Kozi hii itachunguza nadharia kadha za sintaksia. Awali tutaanza na ubainishaji wa kategoria za maneno tukizingatia umuhimu wake katika sintaksia na muundo wa virai au sentensi.

Kozi hii itazingatia zaidi nadharia za msingi za sintaksia kama vile sarufi miundo virai, sarufi zalishi, Nadharia ya ungoekaji na uambatishaji (government and binding). Katika kozi hii virai na sentensi vitachanganuliwa ili kubaini miundo yake. Malengo ya kozi Katika kozi hii wanafunzi wanatarajiwa kufanya yafuatayo: a) Kuelewa maana ya sintaksia b) Kutambua kategoria kuu na kategoria ndogo za sintaksia c) Kueleza umuhimu wa kategoria za sintasia katika kujifunza sintaksia d) kufahamu nadharia mbalimbali za sarufi miundo:Sarufi miundo virai, sarufi patanishi na uteuzi na nadharia X-bar e) kuchanganua sentensi kwa mujibu wa nadharia za sarufi miundo Maudhui ya kozi 1.0 Maana ya lugha na sarufi Lugha ni nini? Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zinazotumiwa na watu ili kupashana habari Sarufi ni nini?

Sarufi ni mfumo wa kanuni za lugha zilizo katika ubongo wa mzawa wa lugha ambazo humwezesha kutunga sentensi zisizo na kikomo ambazo hukubalika na wazawa wa lugha wanaoifahamu lugha hiyo barabara 2.0 Umilisi na utendi wa lugha a) Umilisi ni uwezo wa kuzungumza lugha kwa ufasaha alio nao mtu unaotokana na yeye kuzifahamu vilivyo kanuni za kisarufi hata kumwezesha kuzalisha tungo nyingi zisizo na kikomo. B) Utendi ni utumiaji wa lugha katika mazingira halisi ambao huweza kuathiri maana za maneno kulingana na matumizi yake au na mambo yanayomhusu mzungumzaji mwenyewe k.v. Kutokuwa makini au kukosa kumbukumbu, kuongea akiwa amekasirika, kasoro za ala za sauti k.v. Mapengo, kigugumizi n.k.

Mixmeister Fusion Video 7.0.5 Serial By Dj Nilo. 3.0 Tungo za Kiswahili na Vipengele vyake Lugha ya Kiswahili ina tungo na vipengele mbalimbali kama zilivyo lugha nyingine. Tofauti yake na lugha nyingine zisizohusiana k.v. Kiingereza au Kimasai ni kwamba huhitilafiana katika uundaji wa maneno na mpangilio wa maneno katika tungo. Mathalani, wingi katika Kiingereza hudhihirika mwishoni mwa nomino ilihali katika Kiswahili na lugha dada za Kibantu huonekana mwanzoni mwa nomino. Isitoshe, kivumishi katika Kiswahili hufuata nomino, lakini katika Kiingereza hutangulia nomino.

Kwa hivyo japokwa lugha zote zina maneno, virai,vishazi na sentensi, kila moja ina miundo na vipengele vya kisarufi tofauti na lugha nyingine. 4.0 Kauli za vitenzi na aina zake Kauli ni uhusiano ulipo baina ya kiima na kitenzi (mtenda) au kiima kitenzi na yambwa (mtenda) Aina za kauli Kauli ya kutenda, kutendwa, kujirejea, kutendana, kutendeka, 5.0 Sentensi na aina zake Sentensi ni kifungu cha maneno chenye maana kamili chenye muundo wa kiima na kiarifu a) Sentensi sahili Sentensi sahili ni tungo yenye mana kamili inayoundwa na KN + KT, na ambayo KT ndicho muhimu katika tungo kwani chaweza kusimama peke yake. Miundo ya Sentensi sahili: i) Muundo wa kirai kitenzi (KT) ii) Muundo kirai nomino na kirai kitenzi (KN+KT) iii) Uchanganuzi wa sentensi sahili b) Sentensi ambatani Hii ni sentensi ambayo hundwa na vishazi huru viwili au zaidi kwa kuunganishwa na viunganishi na, lakini n.k. Miundo ya sentensi ambatani i) Miundo yenye vishazi sahili ii) Miundo yenye vishazi sahili + changamani iii) Miundo yenye vishazi changamani pekee iv) Miundo yenye vishazi visivyokuwa na viunganishi v) Uchanganuzi wa sentensi ambatani c) Sentensi changamani Hii ni sentensi yenye kuundwa na kishazi huru na kishazi tegemezi Miundo ya sentensi changamani i) Miundo yenye vishazi rejeshi ii) Miundo yenye vishazi – vielezi iii) Uchanganuzi wa sentensi changamani 6.0 Kategoria za kisarufi Kategoria ya kisarufi ni kundi la maneno lenye sifa za kisarufi zinazofanana. Kwa mfano, mtoto, embe, kiti, mti n.k.